BAADA YA KUWATOA AL MERRIKH, TOWNSHIP ROLLERS SASA KUKIPIGA NA YANGA SIKU HII
Na George Mganga
Licha ya kupoteza mchezo wa jana kwa mabao 2-1 dhidi ya Al-Merrikh katika Ligi ya Mabingwa Afrika, Township Rollers ilifanikiwa kusonga mbele katika Ligi ya Mabingwa Afrika.
Rollers imefanikiwa kusonga mbele kutokana mechi ya awali kuibuka na ushindi wa mabao 3-0, hivyo kuwa na aggregate ya mabao 4-2.
Timu hiyo kutoka Gaborone, Botswana, sasa itakutana na Young Africans ya Tanzania katika hatua inayofuata, mchezo ukichezwa nchini, 6 March 2018, siku ya Jummane, ambapo Yanga itakuwa mwenyeji.
Yanga nayo ilifanikiwa kuwaondoa St. Louis FC ya Sychelles kwa jumla ya mabao 2-0 na kufanikiwa kupiga hatua ya kusonga mbele.
Hata Mechi ya Simba VS Al Masry umesema itachezwa March 6,Dar.Kwa hiyo michezo hiyo yote itachezwa siku moja?
ReplyDeleteYanga imeitoa St.Luois kwa idadi ya jumla ya mabao2-1 na siyo 2-0, waandishi mjitafakari au mrudi shule mkapigwe msasa kama kazi imewashinda.
ReplyDelete