February 22, 2018Rais wa Fifa, Gianni Infantino amesema ana imani kubwa kutakuwa na mabadiliko katika uongozi mpya wa TFF pamoja na Serikali ya Awamu ya Tano ya Tanzania.

Infantino ambaye alikuwa nchini kwa ajili ya mkutano mkuu wa shirikisho hilo, amesema wataendelea kusaidiana na Tanzania katika kuhakikisha kuna mabadiliko makubwa.

“Tuko hapa kushirikiana, kusaidiana na kuunganisha nguvu na TFF pamoja na serikali ili kuhakikisha tunafanikiwa.

“Tunataka kubadilisha mambo na kufikia katika njia sahihi kwenda katika mabadiliko na baadaye mafanikio,” alisema.

Aidha, Infantino amesisitiza kupiga vita masuala ya rushwa na kusema yanahitajika kupingwa kwa kuwa ni chanzo cha kukwamisha mambo mengi.

“Yanapigwa vita na tutaendelea kupambana na rushwa. Kwa sasa tunajua kila kinachoingia kinatoka wapi na tunachotoa kinakwenda wapi.

“Fedha ya Fifa kwa sasa ni kwa ajili ya maendeleo ya mpira na si vinginevyo,” alisema Infantino.


1 COMMENTS:

  1. TFF muwekeeni show game moja la vigogo Simba na Yanga japo aone tulipo katoka soka

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV