February 23, 2018


Na George Mganga

Taarifa zinaeleza kuwa Golikipa namba moja wa timu ya Taifa ya Spain na Manchester United, David de Gea (27) anatajwa kuongeza mkataba mwingine wa kuitumikia timu hiyo, hivyo ataondoa uvumi mwingine wa kuelekea Real Madrid. (Times)


Mabingwa mara mbili mfululizo wa UEFA Champions League, Real Madrid, wapo katika mchakato wa kufanya mazungumzo na winga wa Manchester City, Raheem Sterling (23) ambaye anamaliza mkataba wake 2020. Inaelezwa bado hajaanza mazungumzo yoyote ya kuongeza mkataba na timu hiyo. (Mirror)


Tetesi zinasema pia Real Madrid ipo tayari kumuchia mshambuliaji wake kutoka Wales, Gareth Bale (28), katika msimu huu wa majira ya joto. (Independent)


Chelsea ipo kwenye mazungumzo na Nahodha wa Newcastle United, Jamaa Lascelles, ili aje kuimarisha nafasi ya ulinzi katika kikosi chao msimu ujao. (Evening Standard)


Kibibi kizee cha Torino, Juventus FC, wamefikia makubaliano na beki wa kushoto wa Manchester United, Matteo Darmian (28), ili aende kuitumikia timu hiyo. (Calciomercato - Italy)

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic