Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amekasirishwa na kitendo cha wachezaji Ruvu Shooting kucheza kindava.
Simba imevanikiwa kuishinda Shooting kwa mabao 3-0 katika mechi ya Ligi Kuu Bara huku mchezaji wake Emmanuel Okwi akitolewa nje baada ya kuumizwa.
Okwi ambaye ni kinara wa mabao Ligi Kuu Bara, aliumizwa na beki Mau Bofu wa Ruvu Shooting baada ya kumchezea kindava mara mbili na mwisho kuambulia kadi nyekundu.
“Huu si mchezo wa kiungwana, hawa watu wanakuwa kama vile wametumwa au wanafanya hivyo kuwaridhisha watu fulani.
“Hii si sahihi, inaonekana leo waliingia uwanjani wakiwa wamepania kuwaumiza wachezaji fulani walioambiwa. Si sawa hata kidogo,” alisema Hans Poppe ambaye ni mwanajeshi mstaafu.
mpira ni fair play.. sio ubondia kama hao wajeda
ReplyDelete