February 4, 2018



 Kocha Msaidizi wa Simba, Masoud Djuma, aliyedai kwamba atafurahi zaidi kama straika wake Emmanuel Okwi atafunga mabao 30 msimu huu, imemshitua mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe.

Tambwe ambaye anashikilia rekodi ya kufunga mabao mengi zaidi katika msimu wa 2015/16 akifunga mabao 21, baada ya kusikia kauli hiyo ya Djuma alisema; “Siyo kazi rahisi Okwi kufunga mabao 30.” 

 Tambwe alisema ili Okwi ambaye hivi sasa anaongoza kwa ufungaji akiwa na mabao 12, aweze kufikisha mabao 30, anatakiwa kufunga katika kila mechi atakayocheza.

“Siyo kazi rahisi kwa Okwi kufunga mabao 30, kwani mzunguko wa pili ligi huwa ni ngumu sana, kila timu hupambana kuhakikisha inafanya vizuri ili kuwania ubingwa, nyingine zinapambana zisishuke daraja.


“Inabidi Okwi apambane kwelikweli na ajitahidi pia kufunga katika viwanja vya mikoani lakini kama ataendelea kutegemea Uwanja wa Uhuru na ule wa Taifa pekee, itakuwa ni vigumu kufikisha mabao hayo,” alisema Tambwe.

1 COMMENTS:

  1. Tambwe amesema kweli kwamba kufunga mabao 30 si rahisi inabidi Okwi afanye kazi kweli. Kocha wa Simba aliposema atafurahi kama Okwi atafunga mabao 30 alisema hivyo huku akijua kwamba ni kazi ngumu lakini ana imani inawezekana. Ni kweli inawezekana. Simba wanatengeneza nafasi nyingi sana za kufunga hawazitumii vizuri. Laiti kama wataongeza umakini wakatumia asilimia 70 za nafasi wanazozitengeneza uwanjani na Okwi ndiye kinara wa kuzitumia nafasi hizo, basi mabao hayo 18 yaliyobakia yatapatikana. Inawezekana idadi hiyo kufikiwa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic