February 6, 2018




Kiungo mkongwe wa Azam FC, Salum Abubakar maarufu kama Sure Boy amerejea kikosi Azam FC na ataivaa Simba, kesho.

Simba itaikaribisha Azam FC kesho katika mechi ya Ligi Kuu Bara ambayo inawakutanisha mara ya pili baada ya sare katika mzunguko wa kwanza.

Sure Boy aliikosa mechi iliyopita ya Azam FC ilipoitwanga Ndanda FC kwa mabao 3-0 kutokana na kadi nyekundu aliyopigwa katika  mechi dhidi ya Yanga, Azam FC ikipoteza kwa mabao 2-1.



Msemaji wa Azam FC, Jaffar Iddi Maganga amesema kuwa amesema Sure Boy ameisharejea kikosi na tayari yuko vizuri kwa ajili ya Simba.


“Sure Boy amerejea na yuko na wenzake, ninaamini atakuwa kazini kesho dhidi ya Simba kwa kuwa adhabu yake ya kadi imeisha,” alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic