February 10, 2018



Kocha Mkuu wa St Louis ya Shelisheli, Urlie Mathiot amemsifia kipa wake kuwa ndiye alikuwa nyota wa mchezo.



Yanga imeshinda kwa bao 1-0 dhidi ya Washelisheli hao katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika iliyopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Lakini kipa wa St Louis, Michell Rama alikuwa kizingiti kwa wachezaji wa Yanga.

Mathiot amesema, kipa huyo raia wa Madagascar alifanikiwa kuwazuia Yanga kwa kiasi kikubwa licha ya kwamba wamepoteza mchezo.

"Amejitahidi sana, kwa kawaida unaweza usione, lakini aliipanga vema ngome yake na akafanya vizuri sana," alisema.

"Ni mzoefu na anaijua michuano ya kimataifa, hii imetusaidia sana."

Yanga ndiyo ilimiliki mpira zaidi na kufanya mashambulizi mengi zaidi lakini haikufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao mengi zaidi

Lwandamina raia wa Zambia, anaamini wana nafasi ya kurekebisha makosa yao katika machi ya pili wakiwa ugenini na kufanya vizuri.

Lakini Mathiot anaamini wana nafasi ya kufanya vizuri wakiwa kwao Shelisheli katika mechi ya marudiano.


1 COMMENTS:

  1. Yanga itashinda. Wachezaji wa Shelisheli nimewaona hawana stamina. Kama Yanga ingekuwa kwenye ubora wake leo ingeshinda kwa magoli 4 hivi hata zaidi.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic