February 8, 2018



Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi alimaliza mechi dhidi ya Azam FC akichechemea baada ya kuumia.

Hata hivyo, daktari wa timu hiyo amemfanyia uchunguzi na kugundua majeraha yake hayakuwa makubwa na anaweza kuendelea kuitumikia Simba kama kawaida.

“Unajua Okwi walimgonga kweli, lakini baadaye mambo yameenda vizuri. Daktari kafanya uchunguzi na mwisho amemruhusu kuendelea,” kilieleza chanzo.

Wakati Simba walipoulizwa kwamba Okwi aliumia au la, hawakutaka kulifafanua suala hilo. Lakini baadaye daktari alisema wataangalia na kujua kwa wakati ule asingeweza kueleza kitu.


Kutokana na ruhusa hiyo, Okwi ataendelea na mazoezi leo wakati Simba ikiendelea na maandalizi ya kuwavaa Gendamarie ya Djibouti katika mechi ya Kombe la Shirikisho itakauochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Jumapili.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic