BAADA YA AL MASRY KUTUA NCHINI, BANCE AWA GUMZO KWA MASHABIKI
Na George Mganga
Mshambuliaji Aristide Bance anayekipiga katika timu ya Al-Masry ya Misri, amekuwa gumzo kwa baadhi ya mashabiki wa soka nchini kwa kuzungumziwa.
Bance (33) ambaye ni raia wa Burkina Faso, alianza kuzungumziwa na mashabiki haswa wale wa upande wa pili wanaoshabikia Yanga kutokana na namna ananvyoonekana kuwa mkomavu wa sura, pamoja na umahili wake Uwanjani.
Mshambuliaji huyo alianza kuongelewa tangu Al Masry waiondoe Green Buffaloes ya Zambia katika mashindano haya ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa ushindi wa mabao 5-2.
Licha ya kuzungumziwa, mashabiki wa Simba wamekuwa wakijibu mapigo kuwa, licha ya ujio wake watapambana kunyamazisha kelele ambazo wanatambiwa na watani wao Yanga kuwa atawafunga.
0 COMMENTS:
Post a Comment