BAADA YA MAPUMZIKO YA SIKU MOJA, SIMBA WAANZA KUWAWINDA AL MASRY
Na George Mganga
Kikosi cha Simba kimeanza mazoezi rasmi ya kujiwinda dhidi ya Al Masry SC katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika.
Simba wameanza mazoezi hayo katika uwanja wa Bocco Vetarani uliopo pembezoni kidogo mwa jiji la Dar es Salaam.
Simba wataingia kucheza mchezo huo baada ya kuwaondoa Gendarmarie Nationale FC ya Djibout kwa mabao 5-0.
Mechi hiyo itapigwa saa 12:00 jioni Machi 7 2018 katika Uwanja wa Taifa.
0 COMMENTS:
Post a Comment