March 4, 2018



Nahodha wa klabu ya Fiorentina inayoshiriki Ligi Kuu Italy, Serie A, Davide Astori (31) amefariki dunia, uongozi wa klabu umethibitisha.

Astori amefariki akiwa na wachezaji wenzake katika hoteli moja nchini Italy, wakati wakijiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya Udinese FC.

Mchezaji huyo ametwaa mataji 14 katika maisha yake ya mchezo wa soka ambapo alianzia AC Milan na baadaye kuuzwa kwenda Cagliari.

Kifo hiki ambacho hakijajulikana sababu ni nini, kimepelekea mchezo ulipaswa kupigwa leo kati ya Fiorentina na Udinese kuahirishwa na utapangiwa tarehe nyingine.

Nahodha ambaye aliwahi kuichezea pia timu ya taifa ya Italy nafasi ya ulinzi, namba 5.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic