YANGA YAZINDUA HUDUMA YA KUPATA HABARI KWA NJIA YA SMS, YAWAOMBA MASHABIKI NA WAPINZANI KUJIUNGA ILI KUICHANGIA
Uongozi wa Yanga umetangaza kuanzisha huduma ya kupata habari kupitia ujumbe mfupi wa njia ya simu 'SMS'.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa, amesema huduma hiyo itapatika kupitia mtandao wa TIGO.
Mkwasa amesema ili mtu aweze kujiunga anapaswa kuandika neno YANGA na kutuma kwenda namba 15501.
Baada ya kutuma ujumbe huo, gharama itakayotozwa ni kiasi cha shilingi za kitanzania 100 tu.
Shabiki yeyote atakayejiunga na huduma hiyo atakuwa ameichangia klabu hiyo, ambapo fedha hiyo itaweza kutumika kwa ajili ya maendeleo ya klabu.
Mkwasa amewaomba mashabiki wa wote wa Yanga na wale wasio wa Yanga 'Wapinzani' wajiunge na huduma hiyo kwani itawasaidia kupata mchango wao ndani ya timu.
0 COMMENTS:
Post a Comment