Imeelezwa kuwa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limemfungia kucheza soka kwa muda wa miezi 6 mshambuliaji wa Singida United, Daniel Reuben Lyanga, baada ya kusaini mkataba na timu mbili kwa wakati mmoja.
Taarifa kutoka FIFA zinasema Lyanga alisaini mkataba wa miaka miwili na Fanja FC inayoshiriki Ligi Kuu nchini Oman.
Baada ya kujiunga na Fanja, Lyanga alikuja akasaini tena mkataba na Singida United ya Singida na baadaye uhamisho huwa ukaonekana una walakini mpaka FIFA kufikia maamuzi hayo.
Alipotafutwa Meneja Mkuu wa timu hiyo, Ibrahim Mohamed kuzungumzia hilo alisema kuwa: "Bado hatujapata taarifa rasmi kutoka Fifa kuhusiana na kufungiwa huko, zaidi tunachofahamu ni kuwa mchezaji huyo usajili wake ulikuwa na matatizo kati yetu Singida na Fanja, hivyo tusibirie tukipata taarifa za kiofisi ntakutaarifu.
0 COMMENTS:
Post a Comment