HAJI MANARA AHOJI KUACHWA KWA MKUDE STARS, ASEMA NI KUMKOSEA HESHIMA KULIKO CHUPA
Na George Mganga
Afisa habari wa klabu ya Simba, Haji Manara, amehoji kuachwa kwa mchezaji na kiungo wa timu hiyo, Jonas Mkude, kwenye kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars.
Kauli hiyo imekuja kuafuatia kiungo huyo wa Simba, kukosekana katika majina 23 ya wachezaji wa Taifa Stars walioitwa leo na Kocha Salum Mayanga, huku akisema ni kiungo bora nchini kwa sasa.
Haji amesema mpira unachezwa hadharani, kitendo cha mchezaji huyo kuachwa ni kumkosea heshima Mkude kuliko kuikosea heshima chupa.
"Unamuachaje Mkude? Mwisho wa Siku sisi ni Watanzania. Hata kama si makocha lakini soka huchezwa hadharani, najiuliza tena na tena kwa viungo tulionao ni kweli Jonas Mkude hastahili kuitwa kwenye timu hii? Kwa sasa hakuna ubishi Jonas ndio kiungo mkabaaji 'holding midfielder' bora nchini, ni kumkosea heshima kuliko chupa" ameandika Manara.
Kocha wa Taifa Stars, Salum Mayanga, ametaja majina hayo 23 ya wachezaji watakohusika kwenye mechi za kimataifa za kirafiki dhidi ya Algeria na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Mayanga ana matatizo makubwa ya upendeleo. Kuna wakati alikuwa hamtaki kabisa Ajibu wakati yupo vizuri , alipoulizwa alijibu kwamba kuna wachezaji wengi kuliko Ajibu. Leo hii utamwachaje Mkude ukamchague Tomas Ulimwengu na Farid. Huyu hafai kuwa Kocha wa timu ya taifa. Tupate Kocha wa kigeni. Au hata hawa tulionao wa klabu zetu, bora babu wa Singida apewe timu ya taifa kuliko huyu.
ReplyDeleteWewe manara unajua unakera mpka kukuona najickia vbaya, mtu wa aina gani wewe kuropoka ropoka tu kila jambo? Hivi Faisal na mkude nani zaidi? Acha usimba simba wewe. Mwanaume kama mwanamke bwana. Ninyi ndyo mnaharibu timu acha kocha afanye kazi yake.
ReplyDeleteTuna matatizo makubwa kwenye soka letu, kuanzia viongozi, mashabiki na wachezaji hatujitambui wala hatujui soka linataka nini.
DeleteHayo hakuyasema Manara tu bali wengi walistaajabu kuachwa kwa Mkude. Nini manaake ." najisikia vibaya hata kukuona" Jee ndio unajiona umekamilika mwenye maumbile yaliyokamilika? Wewe si mwana riadha na aibu juu yako
ReplyDeleteHivi ni mchezaji gani anawakera makocha wa Simba kuliko Mkude? Nidhamu ni kitu cha kwanza
ReplyDelete