Aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania TFF, Jamal Malinzi na wenzake imesogezwa mbele hadi Machi 15 kufuatia jalada kukwama kwa DPP hali ilioneka kupingwa kwa hoja nyingi na upande wa utetetezi waliokuwa wakiongozwa na Nehemia Nkoko.
Malinzi anashitakiwa kwa makosa ya kugushushi na nyaraka zikiwemo risiti 20 za TFF pamoja na shitaka la utakatishaji fedha kiasi cha dola za kimarekani 375,418 akiwa na washitakiwa wengine ambao ni aliyekuwa katibu wa TFF, Selestine Mwesigwa na Nsiande Mwanga ambaye alikuwa muhasibu wa shirikisho hilo.
Upande wa utetezi umekuwa ukiamini kesi hiyo inachelewa bila ya sababu za msingi.
Kutokana na hali hiyo, upande kwa mara nyingine umeisisitiza mahakama kusaidia suala hilo kupatiwa ufumbuzi.
0 COMMENTS:
Post a Comment