March 14, 2018




Baada kucheza michezo mitano mfululizo na kuambulia pointi tatu tu, Kocha Mkuu wa Singida United, Mholanzi  Hans van Der Pluijm, amefunguka bado washambuliaji wake hawajiamini na mzunguko huu umekuwa mgumu tofauti na awali.

Singida, mchezo wa mwisho kupata pointi tatu ulikuwa ule dhidi ya Mbao FC ambao walishinda mabao 2-1, ilikuwa ni Februari7, mwaka huu. Baada ya hapo alifungwa na Stand United (0-1) na Azam FC (1-0) huku akitoa sare dhidi ya Ruvu Shooting (1-1) na Kagera Sugar 0-0.

Kocha huyo alisema kuwa tatizo limekuwa kwenye sehemu ya ushambuliaji ingawa hata mechi sasa zimekuwa ni ngumu tofauti na mzunguko wa awali.

“Hivi karibuni nimekuwa na tatizo kwenye safu yangu ya ushambuliaji, vijana wangu hawajiamini kabisa na hapa tulipofika sasa ligi ni ngumu na ushindani umekuwa mkubwa, ni lazima tupambane.

“Kwa sasa nimewapa mapumziko vijana wangu lakini tutaendelea kulifanyia kazi eneo la ushambuliaji, maana bila kufunga mabao huwezi kupata matokeo yoyote, hivyo naendelea kufanyia kazi na huu ni mpira lolote linaweza kutokea,” alisema Pluijm.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic