March 13, 2018


Timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars) imeingia kambini katika Hostel za Makao Makuu ya Jeshi la kujenga Taifa (JKT Mlalakuwa), kujiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika kwa Wanawake (AFCON) 2018 nchini Ghana.

Twiga Stars itacheza dhidi ya Zambia (She Polopolo) Aprili 4, 2018 uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na marudiano kufanyika April 8, 2018 jijini Lusaka nchini Zambia.

 Mshindi wa jumla kwa raundi hii atacheza na mshindi kati ya Namibia v Zimbabwe mwezi Mei, na atakayeibuka mshindi atafuzu moja kwa moja kwa Fainali hizo za Wanawake Afrika.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic