March 20, 2018


Kiungo Mfaransa wa Manchester United, Paul Pogba, amesema itakuwa faraja siku moja akicheza soka na nyota wa Kibrazil, Neymar Junior.

Kauli hiyo imekuja kutokana na kukosekana kwa mahusiano mazuri baina ya mchezaji huyo na Kocha wake, Jose Mourinho, ambaye ameshindwa kumpa nafasi ya kuwa sehemu ya kikosi cha kwanza hivi karibuni.

Pogba amesema Neymar anajulikana ni nani na anafanya nini, hivyo itakuwa jambo jema kama atasakata naye kambumbu wakiwa pamoja.

Pamoja na hayo, Neymar Jr naye anatajwa kutokuwa na furahi ndani ya PSG huku taarifa zikieleza anaomba aongezewe mshahara la sivyo ataondoka kwenda kucheza mahala pengine.

Aidha, awali iliriripotiwa nyota huyo wa Brazil anatamani kurejea klabu yake ya zamani, FC. Barcelona huku ikielezwa anajutia maamuzi ya kukimbilia PSG.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic