March 20, 2018


Uongozi wa klabu ya Yanga umeeleza sababu zilizowafanya waondoshwe katika Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers ya Botswana.

Kupitia Afisa Habari wa klabu hiyo, Dismas Ten, amesema sababu kubwa walishindwa kutumia faida ya Uwanja wa nyumbani, kitu ambacho kilipelekea kushindwa kupata matokeo ugenini.

"Ni muhimu kujua umuhimu wa kushinda mechi za nyumbani kwenye mashindano ya kimataifa", alisema Ten.

Aidha, licha ya kutolewa, Ten amesema kuwa mapambano yataendelea kuelekea Kombe la Shirikisho ambalo wameangukia kutoka Ligi ya Mabingwa Ulaya.

"Tumerudi kwenye Kombe la Shirikisho baada ya kutokufanya vizuri ligi ya Mabingwa, maandalizi yanaaza sasa kuhakikisha tunafanya vizuri " aliongeza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic