March 5, 2018


Na George Mganga

Daktari na Mtaalamu wa masuala ya Saikolojia, Chris Mauki, ametoa somo kwa wachezaji wa Simba katika Hotel ya Sea Scape iliyopo jijini Dar es Salaam.

Mauki ametoa somo la namna ya mchezaji anapaswa kujijengea ujasili pale anapokuwa ndani ya uwanja.

Mtaalamu huyo ameeleza namna mchezaji anapaswa kujitambua na kujiamini pindi anapokuwa uwanjani wakati wa mechi ili kuisaidia timu kupata matokeo chanya.

Somo hilo kwa wachezaji wa Simba limekuja kufuatia maandalizi ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya A Masry SC utakaopigwa Jumatano ya wiki hii Uwanja wa Taifa.

Chanzo cha Habari: Chris Mauki Blog


1 COMMENTS:

  1. Haya ndiyo mambo ya kumuongezea mchezaji niliwahi kusrema Klabu hizi kubwa za Simba, Yanga na Azam mbali ya benchi la ufundi lililokamilika, linahitaji pia kuwa na Dietician, namshauri wa wachezaji niliyemuita Counselor, lakini ndiye huyo anayeweza kushauri masuala ya kisaikolojia. Hongera Simba kwa kuanza na hili. Bado mtaalam wa chakula cha wachezaji. Ni muhimu sana.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic