March 22, 2018


Na George Mganga

Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Young Africans, wamepangiwa kucheza na Welayta Dicha FC inayoshiriki Ligi Kuu Ethiopia.

Klabu hiyo inaonekana kutokuwa na msimu mzuri nchini humo kutokana na nafasi waliyo kwenye msimamo wa Ligi. Welayta wapo nafasi ya 8 wakiwa na alama 19 wakicheza jumla ya mechi 15.

Kumekuwa na mitazamo pamoja na maoni tofauti mitandaoni kuhusiana na timu hii, hata nje ya mitandao haswa wengi kujipa matumaini ya kusonga mbele moja kwa moja.

Na awamu hii imekuwa kama bahati kwa Yanga kupangiwa timu kutoka Ethiopia, kwa maana haijatokea kwa muda mrefu hata mara ya mwisho timu za Tanzania kupangiwa taifa hilo sikumbuki ilikuwa ni lini.

Kikubwa kinachopaswa kufanyika kwa Yanga ni kutokushusha silaha chini na kujiamini kuwa wamepita moja kwa moja.

Yanga wasije wakabweteka na kuziweka silaha hizo chini na kusahau kama mpira huwa una aina ya matokeo matatu ya kufunga, kufungwa ama kwenda sare au saluhu.

Mwanajeshi anapoingia vitani hupambana kwa nguvu zote bila kujali anakutana na mpizani mwenye umbo la namna gani, lazima ajitume ili ashinde.

Nakumbuka hata Township Rollers walikuja hivihivi na kuchukuliwa kama mzaha lakini kilichotokea kila mtu anajua, imebaki stori.

Yanga chini ya Mkuu wa Benchi la Ufundi, George Lwandamina inapaswa kuanza kufanya 'SCOUTING' ya wapinzani wao mapema, wafatilie mechi zao ili waweze kupata mbinu za kuwapiku.

Tusilale tukijiamini kuwa kesho yetu itakuwa nzuri na badala yake ikawa mbaya kwenye mboni za macho yetu.

Naitakia maandalizi mema Yanga kuelekea mchezo huo wa kitaifa.

1 COMMENTS:

  1. Muandishi umeongea maneno mazuri sana ila kwa maandalizi ya timu zetu ni ya kufikirika ila hiyo team si ya kubeza maana kuitoa Zamaleik sio mchezo inabidi wavute sox sana, tunawatakia kila la heri katika maandalizi sana yao maana mwaka huu wamepata bahati ya kupangiwa timu za kawaida kuanzia club bingwa hadi katika shirikisho.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic