March 22, 2018



Na George Mganga
 
Mwenyetiki wa zamani wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage, anaamini Yanga watafanya vizuri katika mchezo wao wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Welayta Dicha ya Ethiopia endapo wataonesha nidhamu ya mchezo.

Yanga imepangwa kucheza na timu hiyo kutoka Ethiopia baada ya droo ya jana kuchezeshwa majira ya saa mbili usiku na Shirikisho la Soka Africa (CAF), jijini Cairo, Misri.

Rage amesema mpira wa sasa ni sayansi, akiwataka Yanga waanze kuyasoma mazingira mapema haswa kuangalia utofauti wa hali ya hewa kwa nchi hizo mbili.

"Vema Yanga wakatazama utofauti wa hali ya hewa, kama Ethiopia kutakuwa na ubaridi basi mechi ya nyumbani waicheze mchana".

"Wasije wakaleta masuala ya usamalia wema kuwachezesha jioni, na kama itakuwa ni joto basi waicheze usiku ili kuwanyima nafasi wapinzani" amesema Rage.

Sanjari na hilo, Rage anaamini Yanga wanaweza wakapata matokeo wakipambana kama walivyocheza dhidi ya Township Rollers FC katika mchezo wa marudiano huko Gaborone Bostwana.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic