March 22, 2018



Kiungo wa Simba, Mnyarwanda, Haruna Niyonzima, rasmi anaendelea na mazoezi binafsi kwa kujifua ufukweni baada ya kuwa nje kwa muda mrefu kutokana na kuwa majeruhi.

Niyonzima amekuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi mitatu na alikwenda kuti­biwa nchini India Februari, mwaka huu na kutokana na kusumbuliwa na tatizo la enka.

Kutokana na majeraha hayo, kiungo huyo alishindwa kwenda Misri ambapo wenzake walikwenda kucheza mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Masry.

Akizungumza na Championi Jumatano, Niyonzima alisema kuwa ameanza mazoezi ya kujifua ufukweni ili ku­weza kuimarisha kiwango chake kutokana na kuwa nje kwa muda mrefu.

“Nashukuru Mungu kwa sasa ninaendelea vyema kidogo ndiyo maana nimeanza kufanya mazoezi ki­dogo kidogo ili kuanza kujiweka sawa baada ya kupata matibabu na kuanza kure­jea katika hali yangu.

“Nafikiri muda si mrefu nitaunga­na na wenzangu maz­oezini na naamini kuwa baada ya muda nitavaa tena jezi ya Simba,” al­isema Niyonzima.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic