March 22, 2018


Kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba na Yanga ambao awali ulipangwa kuchezwa Aprili 7, mwaka huu, tayari baadhi ya wachezaji wa timu hizo hawataweza kucheza kutokana na sababu mbalimbali.

Katika msimamo wa ligi hiyo, timu hizo kwa sasa zinatofautiana mabao ya ku­funga lakini zikiwa sawa pointi kwa pointi 46, Simba ipo kileleni ikifuatiwa na Yanga ingawa Simba wana mchezo mmoja mkononi.

Mchezo wa mzunguko wa kwanza uliopigwa Oktoba 28, mwaka jana ambao ulimal­izika kwa sare ya bao 1-1, vikosi vilivyoanza vya timu hizo mbili ni tofauti na vile ambavyo vinatarajiwa kuku­tana mwezi ujao.

Kuelekea mchezo huo, kwa upande wa Simba wache­zaji ambao watakuwa wapya ambao kwa sasa wamekuwa wakicheza kikosi cha kwanza ni Asante Kwasi, Nicholaus Gyan, Shomari Kapombe, Jonas Mkude na John Bocco ambao wote hawakucheza mchezo wa kwanza.

Ambao wameondolewa kwenye kikosi ni Mohamed Ibrahim ‘Mo’, Method Mwanjale, Haruna Niy­onzima, Mzamiru Yassin na Laudit Mavugo, ukiachana na Mwanjale ambaye ameachwa, wengine ni wag­onjwa na wengine hawana nafasi kikosi cha kwanza.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic