NKOMOLA, NINJA, CHIRWA WAKO FITI ASILIMIA 100 KUWAVAA WABOSTWANA KESHO
Wachezaji Yohana Nkomola, Ramadhani Shaibu 'Ninja' wameungana na Thabani Kamusoko na Obrey Chirwa kwa ajili ya mechi ya kesho dhidi ya Township Rollers ya Botswana.
Wachezaji hawakuonekana katika baadhi ya michezo iliyopita katika ligi na mechi za kimataifa kutokana na majeruhi kuwasibu.
Uwezekano mkubwa wa wachezaji hao kesho kucheza dhidi ya Township Rollers upo, kutokana na hali zao kuendelea vizuri kwa sasa
Kueleka mechi hiyo, Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa amesema wachezaji hao wapo fiti kwa asilimia 100 kuwavaa Wabotswana kesho.
Mechi hiyo inatarajiwa kucheza kesho Jumanne kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
0 COMMENTS:
Post a Comment