YAJUE MAMBO MACHACHE KUELEKEA MECHI YA CRYSTAL PALACE DHIDI YA MANCHESTER LEO
Na George Mganga
Kikosi cha Manchester United kimesafiri mpaka Selhurst Park Stadium kwa ajili ya mchezo wa 29 katika raundi ya pili dhidi ya Crystal Palace.
United iliyo nyuma kwa alama 19 dhidi wa vinara wa ligi, Manchester City, itakuwa inapambana kuhakikisha gepu hilo linapungua huku ikiwania kurejea nafasi ya pili endapo itashinda.
Kuelekea mchezo huo jua tu kwamba Crystal palace haijawahi kushinda mchezo wowote kati ya 17 iliyopita ambayo wamekutana katika ligi.
Kiungo mshambuliaji Pau Pogba amefanikiwa kuifunga Palace katika michezo yote ambayo wamekutana tangu ajiunge na Manchester United.
Manchester United itawakosa Phil Jones, Daley Blind, Marouane Fellain, Ander Herrera na Zlatan Ibrahimovic katika mchezo wa leo.
0 COMMENTS:
Post a Comment