OMBI LA MKWASA KWA WAPENZI NA MASHABIKI WA YANGA KUELEKEA MCHEZO WA KESHO HILI HAPA
Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa amewaondoa hofu mashabiki wa Yanga akiwataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi uwanjani kesho.
Mkwasa alisema shabiki ni mchezaji wa 12, hivyo kujitokeza kwa wingi kutaongeza kutoa hamasa kwa wachezaji kupambana.
Aliongeza kuwa, kikosi chao kipo fiti kwa ajili ya mchezo huo, amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi.
Yanga itakabiliana na Township Rollers ya Botswana katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika katika uwanja wa taifa, Dar es Salaam, saa 10 kamili jioni.
Kila la kheri wawakilishi wetu Yanga
ReplyDelete