March 23, 2018


Beki wa Simba, Salim Mbonde, anatarajia kuungana na wachezaji wenzake Jumatatu ya wiki lijalo kwa ajili ya mazoezi.

Mchezaji huyo ambaye hajaonekana Uwanjani kufuatia kuwa majeruhi, alipata ajali ya pikipiki na kupekelea kuumia jicho lake moja.

Mbonde aliumia jicho lilisababisha aondelewe kwenye orodha ya wachezaji wa Simba waliosafiri kwenda Port Said, Misri, kucheza mchezo wa marudiano dhidi ya Al Masry.

Inaelezwa beki huyo amefumuliwa nyuzi ambazo alishonwa kwenye jicho, na kwa namna hali yake ilivyo, Jumatatu atarejea kuungana na wenzake kikosini.

Kurejea kwa Mbonde kikosini kutampa kazi ya ziada kumshawishi Kocha Mfaransa, Pierre Lechntre, ili aweze kumpanga kwenye kikosi cha kwanza, na hii ni kutokana na kukosekana Dimbani kwa muda mrefu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic