March 23, 2018


Na George Mganga

Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Clifford Mario Ndimbo, amesema haoni tatizo kwa Stars kupoteza mchezo wa jana dhidi ya Algeria.

Katika mchezo huo wa kalenda ya FIFA, Stars ilikubali kichapo cha jumla ya mabao 4-1 katika Dimba la Julai 5 jijini Algiers.

Akihojiwa leo na Sports HQ ya EFM, Ndimbo ameeleza kuwa Algeria wapo vizuri zaidi ya Tanzania na ukiangalia kwa namna walivyotuacha hata kwenye ubora wa viwango vya soka duniani ni mkubwa.

Ameongeza kuwa kilikuwa kipimo kizuri zaidi kwa Stars kutokana na utofauti wa ubora wa timu zote mbili, hivyo si tatizo kupoteza mchezo huo kutokana na Algeria kuwa juu ya Tanzania.

Tanzania imeshika nafasi ya 146 kwenye ubora wa soka duniani huku wapinzani waliotufunga jana, Algeria wakiwa namba 60.

Aidha, Ndimbo ameongeza kuwa Watanzania wengi walikuwa wakilalamika Taifa Stars haipati mechi kubwa za kujipima nguvu, huku akisema TFF sasa inapambana kupata mechi kubwa kuliko zile zilizokuwa zimezoeleka mwanzo.

Stars itakuwa ina kibarua kingine cha mchezo wa kirafiki dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, itakayopigwa jijini Dar es Salaam, Machi 27 2018.

1 COMMENTS:

  1. Hii ni njia ya kukinga kifua....ila tufungwe basi hata tuone kitu katika mpira kimebailika hakuna lolote

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic