![]() |
| Wachezaji wa Simba SC wakiwa katika Airport, Cairo Misri, tayari kuanza safari kuelekea Ports Said. |
Kikosi cha Simba kimewasili salama Jijini Port Said, Misri, kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Masry SC.
Kikosi hicho kikiwa na wachezaji 20 pamoja na viongozi 7, kimewasili salama Port Said baada ya kuondoka jana jijini Dar es Salaam majira ya jioni.
Mchezo huo dhidi ya Al Masry SC utapigwa Jumamosi ya Machi 17 2018.








Kila la kheri Simba watu walishawaotoa Sevilla kabla hata hawajaenda Uingereza. Katika soka chochote kinaweza kutokea hasa kama kutakuwa na wachezaji au mchezaji ambae ameamua kuwa surprise wa mchezo kwa kutumia juhudi zao binafsi za ziada kuleta mabadiliko ya mechi. Ila wachezaji wenyewe lazima waambizane na kukubaliana yakwamba..the Great Diffence of any team is the best offence. Washambuliaji wa Simba na viungo wao wanatakiwa kutumia juhudi za ziada kulimiki eneo lao ilikuwapa wakati mgumu mabeki ambao kwa mpira wa sasa ndio waanzishaji wa mashambulizi. Wachezaji wa mbele wa Simba wasije wakakubali kulazamishwa kuhamisha eneo lao la kazi kulihamishia kwenye goli lao badala yake wanatakiwa kuwalazimisha wachezaji wa mbele wa Almasry kurudi nyuma kwenye goli lao kwenda kudifendi. Sio kazi rahisi lakini kwenye jitihada na nia thabiti hakuna kisichowezekana japo si kwa asilimia mia moja lakini jitihada zikifanyika basi utofauti lazima utatokea.
ReplyDelete