March 23, 2018


Klabu ya Yanga imewaomba mashabiki na wanachama wake wajitokeze Uwanjani kwa wingi kuiunga mkono timu hiyo itakapocheza na Welayta Dicha.

Yanga itakuwa ina kibarua dhidi ya Waethiopia hao kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika utakaochezwa Aprili 7 2018 katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Mecchi hiyo itakuwa ya mkondo wa kwanza kabla ya kurudiana na wapinzani wao April 17 2018 huko Ethiopia.

Kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii, Yanga wameandika wao ni kubwa Tanzania, huku ikiwaomba mashabiki waende kuipa hamasa timu siku hiyo.




1 COMMENTS:

  1. Ukiangalia uteuzi wa kocha wa timu ya Taifa kwa mataifa mbali mbali Duniani mara nyingi huangalia uwezo miongoni mwa makocha wake wazalendo na kama vigezo vyao havitosh basi huangalia uwezo wa makocha wa kigeni wanaofanya kazi ndani katika nchi husika na kama makocha hao wa kigeni wa ndani uwezo wao hautoshi basi huangalia uwezo wa makocha wa nchi jirani. Mwalimu wa mpira kuyaelewa mazingira ya eneo analofanyia kazi ikiwemo tabia za wachezaji ni jambo moja muhimu pakupata kuanzia. Sasa kama kweli TFF wanatafuta kocha wa timu ya Taifa basi hawana haja ya kuhangaika kufanya mchakato wala nini kwa sababu makocha wapo kulingana na uwezo wetu na wakatujengea heshima kwa timu yetu ya Taifa. Tulishashuhudia mchakato wa mbwembwe wa kutafuta kocha kwa TTF chini ya Jamali Malinzi na mwisho wa siku tukaletewa kocha yule wa hovyo kabisa kutoka uholanzi. Katika listi yangu ya makocha ambao nahisi watatujengea misingi imara ya timu yetu ya Taifa, naona wapo wengi lakini naanza huyu Mzee mmoja. Ni yule Babu wa kifaransa aliewahi kuifundisha Simba sport club na baadae Stand United ya kule shinyanga. Mzee yule ana kila kitu tunachohitaji kwa timu yetu ya Taifa. (1)Ana uzowefu wa kutosha katika taaluma yake.(2) Anayaelewa mazingira ya wachezaji wa kiafrika nje ndani (3) Ni muumini mkubwa wa soka la vijana na kuwakuza kuwa lulu.(4) Tayari anayaelewa mazingira ya Tanzania(5)Si dhani kama ni kocha wa bajeti kubwa kulingana na majukumu ya timu ya Taifa. (6) Yupo kikazi zaidi kuhakikisha anachokifanya kinaonekana na kinaleta matunda tena kwa muda mfupi.
    Kama yule mzee ni mzima wa afya na hana majukumu yanayombana basi ni moja kati ya Makocha wazuri wenye kuabudu nizamu katika mpira na atatujengea heshima kwenye Timu yetu ya Taifa .TTF wakifaniwa kumchukua yule mzee basi watakuwa hawajapotea hata kidogo.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic