March 5, 2018


Na George Mganga

Klabu ya Simba imetangaza kutarajia ugeni rasmi wa Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba, katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Masry SC kutoka Egypt.

Simba itamkaribisha Tizeba kuongoza maelfu ya mashabiki wataoenda kuipa hamasa timu yao Uwanjani kwenye mechi hiyo itakayowakilisha taifa kwa ujumla.

Simba itakuwa inacheza na Al Masry baada ya kusonga mbele katika mashindano hayo, kufuatia ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Gandermarie Nationale FC ya Djibout.

Mchezo huo utachezwa saa 12 jioni katika Uwanja wa Taifa dar es Salaam siku ya Jumatano wiki hii.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic