March 23, 2018


Baada ya kikosi cha Yanga hivi karibuni ku­tupwa nje ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, kocha mkuu wa timu hiyo, Mzambia, George Lwandamina, amesema kuwa hawatafanya makosa tena kwenye uwanja wa nyumbani katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Jumamosi iliyopita, Yanga iliiaga michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kutandikwa kwa jumla ya mabao 2-1 na Township Rollers ya Botswana katika mechi ilizokutana na timu hiyo.

Yanga ilifungwa mabao hayo katika mechi ya kwanza iliyofan­yika jijini Dar es Salaam na ile ya marudiano iliyofanyika Botswana matokeo yalikuwa ni 0-0.

Akizungumza na Championi Ju­matano, Lwandamina amesema kuwa baada ya kutupwa nje ka­tika michuano hiyo na kuangukia katika ile ya Kombe la Shirikisho Afrika, watahakikisha wanafanya vizuri katika mechi zote watakazo­cheza nyumbani.

Alisema kushindwa kwao kupata ushindi katika uwanja wa nyumbani, ndiyo kumesababisha waondolewe katika michuano hiyo hivyo hawataki tena jambo hilo litokee.

“Tumejifunza na sasa tunajipan­ga kuhakikisha tunafanya vizuri katika mechi za nyumbani, kama tungefanya vizuri katika mchezo wetu wa kwanza tungesonga mbele.

“Vijana wangu walijitahidi sana kupambana katika mchezo wetu wa marudiano dhidi ya Township Rollers lakini tulishindwa kupata ushindi, kwa hiyo katika mechi zetu zijazo ni lazima tufanye vizuri nyumbani,” alisema Lwandamina.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic