March 22, 2018



Na George Mganga

Mechi ya kirafiki iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu kati ya Algeria dhidi ya Tanzania imemalizika kwa wenyeji kuibuka na ushindi mnono wa mabao 4-1.

Mechi hiyo imepigwa usiku huu katika Uwanja wa Mustapha Tchaker huko Blida nchini humo.

Mabao ya Algeria katika mchezo huo ambao waliutawala kwa asilimia kubwa, yalifungwa na Baghdad Bounedjah kwenye dakika za 13 na 80, Shomari Kapombe akijifunga kwa kichwa dakika ya 43 na bao la mwisho likifungwa na Carl Medjan (52').

Bao pekee la Taifa Stars limefungwa na Simon Msuva kufuatia kona safi ya Shiza Kichuya mnamo dakika ya 20.

Matokeo hayo yanaleta taswira mbovu kwa Tanzania haswa kuelekea kupanda kwa ubora wa viwango vya soka duniani.

Kwa mujibu wa kalenda ya FIFA, Stars itakuwa ina kibarua kingine cha mchezo wa kirafiki, dhidi ya  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, mechi hiyo itafanyika jijini Dar es Salaam, Machi 27 2018. 

1 COMMENTS:

  1. TFF na ndoto za alinacha.tuko serious kweli na timu ya Taifa au kupotezeana muda tu?
    timu inaonekana wazi haina benchi la ufundi na makocha wa viwango na kwa staili hii tusitegemee kupandisha viwango Fifa.Leo tena timu yetu tumeonekana kama wanafunzi wa kutoka chuo na kubaki kurukaruka

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic