BAADA YA KUTUA NCHINI, YANGA YAPISHANA NA VIJANA WAO UWANJA WA NDEGE
Wakati Yanga wakirejea nchini usiku wa kuamkia leo ikiwa ni majira ya saa 7, kikosi hicho kitaendelea kuwakosa wachezaji wake, Said Mussa na Ramadhani Kabwili.
Yanga imepishana na wachezaji hao Uwanja wa Ndeje wa Mwalimu Nyerere, baada ya kuondoka mapema leo alfajiri kueleka Congo kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa kufuzu kuelekea AFCON (U20) huko Niger.
Kikosi cha Yanga kiliwasilia majira ya saa 7 usiku wakati Ngorongoro Heroes wakiwa kambini na kuwafanya wasiweze kuonana na wachezaji wenzao Uwanja wa Ndege.
Tayari Ngorongoro Heroes wapo safarini hivi sasa, huku Mussa na Kabwili wakiwa ni miongoni mwa wachezaji walio kwenye msafara wa safari hiyo.
Mussa na Kabwili wataungana na Yanga baada ya kurejea nchini ikiwa tayari wameshakamilisha kibarua cha kufuzu kuelekea AFCON chini ya miaka 20 dhidi ya Congo, zitakazofanyika huko Niger mwakani.
0 COMMENTS:
Post a Comment