WENGER ASEMA SASA INATOSHA, NI NAFASI KWA WENGINE KUCHUKUA MIKOBA YAKE
HATIMAYE Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger, ametangaza kuachia ngazi klabuni hapo baada ya msimu huu kumalizika.
Wenger ameifundisha timu hiyo kwa miaka 22 tangu ajiunge nayo na sasa amefikia maamuzi ya kuamua kuachana nayo baada ya kuinoa kwa muda mrefu.
Wenger amesema alikaa na kutafakari kwa kina kuhusiana na hatma yake na klabu hiyo, ambapo aliamua kukaa na uongozi wa juu wa timu hiyo na kuwaeleza kuwa wakati wake sasa umefikia mwisho.
“Baada ya kutafakari kwa kina kufuatia mazungumzo na klabu yangu, umefika wakati sasa nikae pembeni mwisho wa msimu huu, nina furaha sana kwa muda wote niliokaa hapa klabuni.
“Ninawashukuru wafanyakazi wenzangu, wachezaji, wakurugenzi na mashabiki kwa kuifanya klabu hii kuwa spesho, nimeitumikia kwa miaka mingi” amesema Wenger kwenye taarifa yake rasmi leo Ijumaa.
0 COMMENTS:
Post a Comment