Kipa namba wa Singida United, Ally Mustapha ‘Barthez’ anatarajiwa kukaa nje ya uwanja siku saba akiuguza maumivu ya pembeni mwa kifua chake.
Kipa huyo aliyewahi kuzidakia Simba na Yanga, atakaa nje ya uwanja baada ya kupata majeraha hayo kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara iliyochezwa jana katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Timu hizo, zilitoka sare ya bao 1-1 katika mchezo huo huku bao la kuongoza la Singida likifungwa Kambale Salita huku la kusawazisha likipachikwa na Shaibu Ramadhani ‘Ninja’.
Akizungumza na SALEHJEMBE, Meneja Mkuu wa Singida, Ibrahim Mohamed alisema kipa hao atakaa nje ya uwanja kwa muda huo baada ya kugongana na mchezaji wa Yanga.
Ibrahim alisema, kipa huyo alishindwa kufanya mazoezi ya leo Alhamisi asubuhi kutoka na majeraha hayo aliyoyapata kwenye kifua.
“Barthez atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa siku saba akiuguza majeraha ya sehemu ya pembeni ya mbavu ambayo alionekana kulalamikia maumivu huku ikiwa imevimba, hivyo baada ya vipimo ikaonekana kapata maumivu hayo,” alisema Ibrahim.
0 COMMENTS:
Post a Comment