April 17, 2018



Nahodha na beki kisiki wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, amesema kuwa mechi yao na watani wao, Simba wala haina umuhimu kwao kutokana na wao kuwaza fedha ambazo wataingiza baada ya kutinga katika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga wanaoshika nafasi ya pili kwenye ligi wakiwa na pointi 47 watakutana na Simba katika pambano la ligi ambalo linatarajiwa kupigwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar Aprili 29, mwaka huu ambapo pambano hilo ndilo litatoa taswira juu ya timu ipi itat­waa ubingwa kwa msimu huu.

Pia kikosi hicho cha Yanga kilisafiri usiku wa kuamkia jana Jumapili kuelekea Ethiopia kwa ajili ya kwenda ku­vaana na wenyeji wao Wolatya Dicha katika mchezo wa mkondo wa pili wa Kombe la Shirikisho Afrika ambao utapigwa nchini humo keshokutwa Jumatano.

Cannavaro ambaye ameiongoza Yanga kutwaa ubingwa misimu mi­tatu mfululizo, ameliambia Cham­pioni Jumatatu, kuwa mchezo wao dhidi ya Simba wala hauwau­mizi kichwa kutokana na kutokuwa muhimu sana kwa kuzingatia mwenendo wa ligi ulivyo bali wana­chokiangalia kwa sasa ni mechi ya marudiano na Dicha ambapo kama wakifuzu hatua ya makundi wa­takunja kiasi kikubwa cha fedha.

“Hiyo mechi na Simba kwa sasa siyo muhimu sana kwa sababu kwanza iko mbali tofauti na mchezo wetu huu wa marudiano dhidi ya Dicha ambao kama tukifanikiwa kusonga mbele kuna donge kubwa la fedha ambazo tutazipata tofauti na tukikomaa na ligi.

“Kwangu mimi naona ni bora tukiweka akili zetu juu ya mechi hiyo ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Wolayta Dicha na siyo kitu kingine, tukimalizana nao ndipo tutaanza kufiki­ria juu ya mechi zijazo za ligi,” alisema Cannavaro.

Iwapo Yanga itafanikiwa kusonga mbele kwenye hatua ya makundi ya kombe hilo la shirikisho Afrika itakuwa imejiingizia fedha katika nafasi yoyote ile ambayo watashika. Ikiwa ya nne katika kundi itapata milioni 336, wa tatu milioni 536, wa pili milioni 536 au wakiwa mabingwa wa kombe hilo watajikusanyia bilioni 1.8.

CHANZO: CHAMPIONI

5 COMMENTS:

  1. Jee hizo pesa anazoongelea huyo mpiga porojo ikiwa watazipata zitawatosha kuwalipa mishahara ya miezi mine ili mipate angalau morali ya kusimama mbele ya mnyama hatari?

    ReplyDelete
  2. Maelezo ya CANNAVARO yanaonesha jinsi gani Yanaga ilivyokwisha kata tamaa na ubingwa kwani hata Yanga akishinda mechi na waisiopia ni ndoto kwenda kuchukua ubingwa wa mashindano hayo na wakitolewa katika mashindano hayo hakuna njia nyengine yeyote ile ya kurudi tena kwenye mashindano hayo kama si kuishinda Simba katika kubeba ubingwa wa Tanzania sasa vipi match ya simba iwe haina umuhimu kwa yanga?

    ReplyDelete
    Replies
    1. kuna tsh milioni 600 za caf. Sport pesa milioni 400 na Macron m.53 unataka nn zaid ya hapo? na hizo sio ukichukua ubingwa hapana ukiingia tu makundi.

      Delete
  3. Canavaro ataka pesa kuliko kingine connotethe

    ReplyDelete
  4. mmesahau hizo pesa mnapewa ili kuwawezesha kujiandaa na hiyo atua ya makundi?mnawaza kugawana tu,timu inamadeni,bd mnatakiwa kujiandaa.kubalini mzipate ila muwe mmejitolea sadaka,maana mtaaibika mkiwaza kugawana.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic