April 23, 2018



Shirikisho la Soka Tanzania Bara (TFF) limetoa ufafanuzi kuhusiana na klabu ya Mtibwa kama itaweza kushiriki mashindano ya kimataifa endapo itakuwa bingwa wa Kombe la Shirikisho.

Ufafanuzi huo umetolewa kutokana na Mtibwa Sugar iliwahi kufungiwa baada ya kushindwa kusafirisha timu kutokana na ukata miaka ya nyuma.

TFF wameeleza kuwa endapo Mtibwa atakuwa bingwa watakachokifanya ni kuwasilisha jina la mshindi CAF kisha wkusubiri majibu.

Shirikisho hilo limesema ni mapema zaidi kutoa majibu rasmi kwa maana watategemea CAf itasema nini, kama wakitaka timu ibadilishwe itabidi iwe hivyo.

Mtibwa imeshatinga hatua ya fainali ya mashindano ya Kombe la Shirikisho kwa kuitwanga Stand United mabao 2-0.

Mshindi wa mashindano haya ataiwakilisha Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho Afrika huku bingwa wa ligi akishiriki Ligi ya Mabingwa.


CHANZO: EFM RADIO

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic