April 27, 2018


SIKU YA PILI (JANA)


Kocha mpya wa Yanga, Mwinyi Zahera amejikuta akilazimika kubadili mavazi yake siku yake ya pili akiwa kazini.

Siku ya kwanza alianza mazoezi ya kuinoa Yanga mjini Morogoro akiwa na jezi iliyokuwa na rangi nyekundu ambazo ni rangi za watani wao Simba.
Hali hiyo ilionekana kuwakera mashabiki wengi wa Yanga hasa ikizingatiwa kuwa wanakwenda kucheza nao Jumapili.

Zahera hakuona shida kwa kuwa ilikuwa ni sehemu tu ya jezi yake ambayo ni ya timu yake ya taifa DR Congo ambayo bendera yao ina rangi nyekundu.

Jana ambayo ilikuwa ni siku ya pili, Zahera alioenakana akiwa na jezi nyingine ambazo inaelezwa zilitafutwa “haraka iwezekanavyo.”

Kocha huyo alianzisha gumzo baada ya kupiga picha yake ya kwanza nchini akiwa amevaa suti yake nadhifu na tai nyekundu.

Tai hiyo iliibua mjadala na hasa mitandaoni lakini baadhi ya mashabiki wa Yanga wakasisitiza kuwa “si ishu kiivyo”.


SIKU YA KWANZA (JUZI)

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic