April 15, 2018




Kikosi cha Yanga kipo angani hivi sasa kuelekea Ethiopia kwa ajili ya mchezo wa mkondo wa pili wa Kombe la Shirikisho dhidi Wolaiita Dicha FC utakaopigwa Aprili 18 2018.

Katika orodha ya wachezaji walioondoka leo, Yanga imewakosa Andrew Vincent, Ramadhani Kabwili, Said Mussa na Ibrahim Ajibu.

Ajibu amesalia kutokana na hali yake kuwa kutoruhusu huku Kabwili na Mussa wakiwa na majukumu kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes.

Wakati huohuo Andrew Vincent naye amebaki nchini kutokana na hali yake bado haijaimarika baada ya kuumia katika mchezo uliopita dhidi ya Wolaitta Dicha uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

1 COMMENTS:

  1. Ajibu sema wazi bila kuficha kilichokuzuwia kujiunga na timu yako uliyoipenda kwasababu msemakweli ni kipenzi cha Mungu. Piga hodi urejee nyumbani ulipolelewa na kukufikisha hapo ulipokuwa kabla hujaihama hiyo nyumba.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic