April 1, 2018













Penati ya 5 Singida wanapiga, anapiga Sumbi,gooooli Singida wanapita, Sumbi anaifungia Singida United penati ya 4 na kuifanya ifuzu kuingia hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho

Zamu ya Yanga, wanapiga penati ya nne, anapiga Martin, piga pale, inakwenda nje, amekosa
Kenny Ally anaenda kupiga penati ya nne kwa Singida, anapiga, goooli wanapata

Yanga sasa wanapiga ya penati ya tatu, Gadiel Michaeeeel, Piga pale gooooli, Yanga wanapata
Singida wanapiga penati ya tatu, Kutinyu, anapiga goooli, wanapata

Penati ya pili kwa Yanga anaenda kupiga Yondan,  piga goooooli, wanapata
Singida wanaenda kupiga penati ya pili, pigwa pale, Singida wanakosaa

Yanga wanafuata, wanaanza penati ya kwanza, kipa Mustapha yupo langoni, Tshishimbi anaenda kupiga, pigaaaa, inakwenda nje, Yanga wanakosa tuta la kwanza
Singida wanaanza kupiga, Batambuze anapigam goooli, wanapata penati ya kwanza

Hatua ya matuta inafuata

MPIRA UMEKWISHA, SINGIDA UNITED 1-1 YANGA 

Dak ya 92, Singida wanafanya mabadiliko, ameingia Sumbi
Dak ya 91, Sekunde tu zimesalia mpira kumalizika, hatua ya matuta itafuata
Dak ya 91, Nizar na mpira, kwake Kiggy Makasi engo ya kushoto mwa Uwanja, goli kiki

DAKIKA 90 ZIMEMALIZIKA, MBILI ZIMEONGEZWA

Dak ya 89, Pigwa hukuu Yanga wanaokoa na kupiga Counter Attack, mpira unakwenda nje
Dak ya 88, Kona inapigwa kuelekea Yanga, inapigwa, kona nyingine
Dak ya 87, Imetokea hatari kwenye lango la Yanga, juhudi za Rostand zimesaidia kuokoa bao, bado ni 1-1
Dak ya 86, Makasi na mpira, kwake Batambuze
Dak ya 85, Ajib anapiga, unatua mikononi mwa Mustafa kiulaiini kabisa
Dak ya 84, Yanga wanapata faulo nyingine nje kidogo ya eneo la hatari, Singida wanapaswa kuwa makini haswa dakika hizi za mwisho
Dak ya 83, Juma Abdul anatoka na nafasi yake inachukuliwa na Hassan Kessy
Dak ya 82, Goli Kiki, Rostand anapiga moja ndeefu inaenda moja kwa moja nje
Dak ya 81, Yanga wako langoni mwa Singida, pigwa huku Singida wanatoa nje, Juma Abdul anarusha
Dak ya 80, Faulo nyingine inapigwa kuelekea lango la Singida, inapigwa lakini kipa Barthez anaudaka
Dak ya 78, Chirwa anashindwa kumalizia vema kazi nzuri ya Tshishimbi, anaupalaza mpira unakwenda nje, goli kiki

Dak ya 75, Piga huku lakini mabeki wa Singida wanaokoa, unarudi kwa Ajib tena unambabatiza na kutoka nje
Dak ya 75, Yanga wanapata faulo, anapiga Ajib, ni sehemu nzuri endapo akitulia anaweza kuipatia Yanga bao la pili
Dak ya 74, Cheza huku Ajib, Nizar anakataa, unakuwa wa kurushwa kuelekea lango la Singida
Dak ya 73, Dakika zinazidi kuyoyoma, mpira unaendelea na Singida wameonekana kumilizi zaidi mpira
Dak ya 72, Kevin Yondan anazozana na mchezaji wa Singida, tafurani kidogo inatokea
Dak ya 71, Dante analambwa kadi ya njano, ni kadi ya kujitakia, faulo inapigwa, pigwa huku lakini mpira unaokolewa

Dak ya 69, Mpira umesimama kidogo, Kocha Hans anajaribu kupeana mawaidha na wachezaji wake kidogo
Dak ya 67, Offside, Mwamuzi wa pembeni ananyanyua kibendera baada ya Chirwa kuotea
Dak ya 66, Chukua Chirwa sasa, anakimbia na mpira, hesabu zake zinakataa mpira unakwenda nje
Dak ya 65, Emmanuel Martin anaingia kuchukua nafasi ya Juma Makapu
Dak ya 63, Mpira anao Chikupe, anapasia kati huku lakini unaokolewa
Dak ya 62, Singida wameamka, wanashambulia lango la Yanga kama nyuki
Dak ya 62, Rostand anaanza upya baada ya mpira kutoka nje
Dak ya 61, Yanga wanatoa nje, Singida wanarusha

Dak ya 61, Mhilu sasa anakwenda na mpira, penyeza kwake Ajib, anapiga krosi huku lakini inaokolewa na Kiggy Makasi
Dak ya 60, Kotinyu anang'aa zaidi eneo la kati hii leo, amekuwa mtulivu kwa dakika zote pale anapopata mpira
Dak ya 55, Singida United 1-1 Yanga
Dak ya 53, Singida bado wanaumiliki wa wingi eneo la kati, chukua sasa Yanga huku, wanakwenda nao, kwake Yusuph Mhilu, piga moja huku inakwenda nje
Dak ya 52, Hali ya hewa imetulia sasa, mvua imekata
Dak ya 51, Singida wameamka zaidi, bao la kusawazisha limewapa morali
Dak ya 50, Hatariii katika lango la Yanga, nafasi Singida wanakoa hapa, ni kona
Dak ya 47, Goooooli, Kenny Ally anaisawazishia Singida United ni 1-1 sasa
Dak ya 45, Mpira umeanz. Singida wanafanya shambulizi kali dakika hii ya kwanza kipindi cha pili, mpira unakwenda nje

DAKIKA 45 ZA KIPINDI CHA PILI ZIMEANZA

DAKIKA 45 ZA KWANZA ZIMEMALIZIKA, SINGIDA 0-1 YANGA

Dak ya 44, Kutinyu anapewa kadi ya njano, ni ya kwanza katika mchezo huu
Dak ya 43, Kona inapigwa kuelekea Yanga, Kiggy Makasi anapiga lakini inatua kwa kipa Rostand
Dak ya 43, Faulo nyingine anachezewa mchezaji wa Singida, inapigwa na Mudathir Yahaya, piga kubwa huku lakini inaokolewa
Dak ya 42, Ajib amechezewa madhambi, inakuwa faulo kuelekea Singida United
Dak ya 40, Kona inapigwa kuelekea Singida, anapoga Ajib, anaanza kwa kumpasia Gadiel, Gadiel anamwachia Ajib anapiga shuti moja kuubwaa na kwenda nje kwa mashabiki
Dak ya 39, Goli Kiki, mpira unapigwa kuelelea Singida United. Yanga wameshaanza sasa, kwake Tshishimbi, Singida wanauchukua

Dak ya 38, Tayari kona ishapigwa lakini inakosa madhara
Dak ya 37, Kutinyu sasa, anabanwa na mabeki lukuki wa Yanga, kwake Nizar, inapigwa krosi moja kulia mwa Uwanja, Dante anatoa nje, kona
Dak ya 36, Khalfan na mpira, pasia kwake Kotinyu, gawa pembeni huku Kennedy, inapigwa moja hukuuuu, nje
Dak ya 35, Mpira unatoka nje, Gadiel anarusha, rusha kumtafuta Chirwa lakini anatumia nguvu na inakuwa faulo kuelekezwa Yanga
Dak ya 34, Mvua inaharibu ladha ya mpira, maji yameanza kujaa Uwanjani
Dak ya 33, Faulo inapigwa kuelekea Yanga, anapiga Shafik Batambuze

Dak ya 32, Imepigwa lakini inaokolewa kwa kichwa na mabeki wa Singida
Dak ya 31, Kona nyingine inapigwa kuelekea Singida
Dak ya 30, Mudathir na mpira sasa, piga mbele Dante anaokoa
Dak ya 30, Inapigwa kona kuelekea Yanga, pigwa huku lakini kichwa cha mchezaji wa Singida kinashindwa kuupiga vizuri mpira na kwenda nje
Dak ya 29, Mvua inazidi kunyesha uwanjani
Dak ya 27, Hatari katika lango la Yanga, pigwa krosi kali na Kutinyu lakini mpira unavuka lango

Dak ya 25, Singida wanarusha baada ya Yanga kuutoa, unarushwa kwake Kontiyu, kwake Nizar Khalfan, piga shuti kali unagongwa kichwa unarudi dimbani
Dak ya 24, Kona inapigwa kuelekea Yanga, namna gani Singida wamekosa nafasi ya kupasia kamba, matokeo ni 0-1
Dak ya 23, Inapigwaa, Gooooooooal, Yusuph Mhilu anaiandikia Yanga bao la kwanza kwa njia ya kichwa
Dak ya 21, Mpira unarushwa kuelekea Yanga, kwake Chikupe, piga mbele huku, hataari, kona, inaelekezwa Singida United

Dak ya 20, Gadiel Michael anaondolewa nje ya uwanja baada ya kuumia, mpira unaendelea
Dak ya 19, Kona, Singida wanapata kona ya kwanza, Makasi anakwenda kupiga, piga huku lakini inaokolewa
Dak ya 18, Chikupe anapasia nyuma ya goli, unamkuta kipa Rostand anapiga nje, ingeweza kuwa hatari kwa Yanga
Dak ya 16, Ajiiib, piga pasi moja ya kunyanyua lakini inakosa mmaliziaji na kutua kwa Barthez kiulaiini
Dak ya 15, Jukwaa la VIP watu wanalowa na mvua inayoendelea kunyesha
Dak ya 14, Kutinyu sasa katikati mwa Uwanja, piga kwake Makasi, Makasi anampasia Mudathir Yahaya, faulo, anachezewa Nizar Khalfan

Dak ya 13, Makapu anapiga mbele kuwatafuta washambuliaji, mpira unakosa mtu, Singida wanauchukua na kuanza upya
Dak ya 12, Andrew Vincent anatolewa nje ya dimba kugangwa baada ya kuumia
Dak ya 10, Ajib anakosa nafasi ya kupachika bao, ilikuwa ni shambulio zuri kwa Yanga, mpira unaendelea
Dak ya 8, Kimvua kinanyesha uwanjani, kila timu inapambana kutafuta goli la mapema
Dak ya 6, Batambuze anaanza kati, piga pasi pembeni huku na mpira unatoka, faulo, inapigwa kwenda Yanga. Imepigwa huku mbelee, kipa Rostand anadaka kama mboga, haikuwa na madhara

Dak ya 5, Faulo imeshapigwa, inagongwa kichwa na wachezaji Singida na kurudi katikati mwa dimba, Tshishimbi anauchukua tena
Dak ya 4, Tshishimbi anachezewa madhambi, inapigwa faulo kuelekea Singida
Dak ya 3, Singida wamepata shambulizi kali la kwanza, lakini linashindwa kuzaa bao, bado 0-0
Dak ya 2, Singida wanaukokota katikati mwa Dimba, Kotinyu anapiga pasi mbele huku lakini Yanga wanaokoa
Dak ya 2, Mpira umeanza punde huku mvua ikiwa inanyesha Uwanja wa Namfua
Dak ya 1, Mpira umeanza

1 COMMENTS:

  1. Yaleyale Simba nje, Azam nje, Yanga nje. Safari hii tutapata mwakilishi kutoka mikoani. Kipi mlichomcheka Simba?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic