Djako anaichezea Dicha SC iliyotoka kuondolewa na Yanga katika fainali za Kombe la Shirikisho Afrika juzi Jumatano.
Inaelezwa kuwa Yanga ina mkakati wa kumsajili Djako pengine kuja kuziba pengo la Donald Ngoma ama Amis Tambwe ambao wamekuwa majeruhi wa muda mrefu.
Uwezekano mkubwa wa Yanga kumsajili mchezaji huyo upo, na hii ni baada ya kutwaa kitita cha zaidi ya milioni 600 kufuatia kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho.
Tetesi za ujio wa Mshambuliaji Djako zimeanza ikiwa zimesalia siku kadhaa kuelekea mechi ya watani wa jadi kati ya Simba na Yanga itakayopigwa Aprili 29 2018
Kikosi cha Yanga kimewasili usiku wa kuamkia leo kikitokea nchini Ethiopia kwa ajili ya kushiriki mashindano hayo.
0 COMMENTS:
Post a Comment