April 19, 2018



Baadhi ya mashabiki wa klabu ya Yanga wameanza kuwatupia vijembe wenzao wa Simba kutokana na kutinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa kuiondoa Wolaita Dicha SC.

Kusonga mbele kwa Yanga kumeiwezesha kutwaa kitita cha zaidi ya shilingi milioni 600 ambazo hutolewa kwa kila timu inayofuzu kuingia hatua hiyo.

Kejeli na majigambo kwa mashabiki wa Yanga hivi sasa ni kuhusu fedha hizo ambazo watakabidhiwa kufuatia kutinga kwenye makundi, wapo wanaoeleza kuwa zina thamani kuliko ubingwa wa ligi kuu nchini.

Mashabiki hao baadhi wamekuwa wakiwatupia vijembe watani wao wa jadi, Simba, wakisema kuwa thamani ya ubingwa wa ligi ni milioni 80 pekee, tofauti na kutinga hatua ya makundi kwenye Kombe la Shirikisho (CAF Confederation CUP)

Wapo baadhi wanaamini ubingwa kwao inaweza kuwa ndoto hivyo wamefarijika na kufurahia kutwaa kitita hicho cha fedha ambazo zitatumika kwa matumizi mbalimbali ya klabu.


4 COMMENTS:

  1. Naam hicho ndicho wanachokishanglua kwasababu wanashida nazo lakini wametandikwa na wasisahaukuwa Mnyam, Shooting, Prson na Mtibwa wanakungojeeni tena ugenini na baadae kimbunga cha kukimbiwa na nyota wenye njaa

    ReplyDelete
  2. Pesa ilileta shida mbeya city,stend United,natarajia watu kugoma ikitokea hawatalipwa wanachostahili kwani katika hiyo pesa kuna madeni muhimu,huku wachezaji wakiwa namatumaini ya mishahara,naiona ile hadithi ya kifaranga utanyonya kesho.hii pesa ishaleta tabu jangwani tusubiri tuone

    ReplyDelete
  3. Heheee Yanga buanaa.. haya yetu macho na masikio maana sidhani kama bakora za mzee Akilimali zitawaacha salama.

    ReplyDelete
  4. They are all out to get money that they failed to get since long away. Where will that money go? Lets wait and see if it is not going to generate confusion among players who have gone too long without money

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic