April 19, 2018



Baada ya kunyakua mamilioni kutoka CAF kutokana na kuindoa Wolaita Dicha SC kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika jana, Yanga sasa inahamishia silaha zake Ligi Kuu Bara.

Yanga imefanikiwa kusonga mbele kwenye mashindano hayo na kutinga hatua ya makundi kwa idadi ya mabao 2-1 dhidi ya Waethiopia hao.

Katika mchezo wa kwanza ukiopigwa jijini Dar es Salaam, Yanga iliibuka na ushindi wa mabao mawili kwa sifuri, na jana ikakubali kichapo cha bao 1-0.

Kufuatia matokeo hayo, Yanga itaanza safari leo ya kurejea nyumbani ambapo mchezo wake wa ligi utakaofuata ni dhidi ya Mbeya City FC utakaopigwa mjini Mbeya kwenye Uwanja wa Sokoine.

Yanga inarejea kuja kufukuzia ubingwa ikiwa nyuma kwa alama 11 dhidi ya watani wao wa jadi, Simba SC, walioukosa ubingwa huo kwa takribani miaka mitano mfululizo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic