April 19, 2018



Afisa Habari wa timu ya soka ya Simba Haji S. Manara, amesema kwamba anaamini kuwa siku moja ndoto yake ya kuwa Rais wa Tanzania itakuja timia, kwani ndio tamanio lake la siku nyingi.

Akizungumza kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa kupitia ukurasa wa facebook wa East Africa Television, Haji Manara amesema yeye kama mwanasiasa upande wa pili, ndoto yake kubwa ni kuja kuwa Rais wa nchi baada ya kuzichanga.
“Iko siku mungu akinipa majaliwa, nikazichanga karata zangu, nitakuja kuwa rais, ndiyo ndoto yangu, na ndio ndoto za wanasiasa wote duniani, unaona bunge lile!? kama kuna mwanasiasa ambaye hana ndoto ya kuwa Rais hawafiki watano, mwanasiasa yoyote ukishaingia, hizo ndio ndoto kuja kushika wadhifa wa juu, kama huna ndoto wewe hufai kuishi”, amesema Manara.
Kauli hiyo ya Manara sio mara ya kwanza kusikika akiitamka, huku akisistiza kwamba kwa kuwa yeye ni mwanasiasa mzuri na mkweli, pia ni kada wa CCM, anaamini atakuja kushika wadhifa huo mkubwa kwenye nchi.

CHANZO: EAST AFRICA TV

1 COMMENTS:

  1. Una haki ya kuongea lolote la maadili mema lkn kama utapata nafasi hiyo wananchi wote watakuwa mahayawani, labda kwa wasuokufahamu, cv yako imeharibika kwa matukio yako maovu ulupokuwa katibu mwenezi wa ccm wa mkoa wa DSM, ulitumia cheo chako vibaya

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic