April 30, 2018



Mchezaji wa zamani wa Yanga, Bakari Malima maarufu kama Jembe Ulaya, amemtupia lawama beki Hassan Kessy baada ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwenye mchezo wa ligi dhidi ya watani zao wa jadi Simba.

Kessy aliondolewa nje kwa kupewa kadi ya pili ya njano na Mwamuzi kufuatia kitendo cha kumchezea rafu beki wa Simba, Asante Kwasi ikiwa ni kipindi cha pili cha mchezo.

Kuafuatia tukio hilo kutokea, Malima amesema kuwa Kessy bado ana utoto mwingi kitu kinaweza kupelekea timu kugharamika mchezoni.

Malima ameeleza kitendo alichokifanya Kessy hakikuwa cha kiungwana na kinapaswa kukemewa huku akieleza alipaswa kuonesha utulivu na si kuonesha mpira wa ajabu uliopelekea aondolewe kizembe Uwanjani.

Hata hivyo, Malima ameeleza pia kuwa mchezo wa jana kwa Yanga ulikuwa umepooza sana na kusema Simba walistahili kushinda kutokana na aina ya mpira walioupiga.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic