MKWASA ATAJWA KAMA SABABU YA LWANDAMINA KUTIMKA YANGA, KAMATI KUKETI LEO BAADA YA MECHI NA SINGIDA
Taarifa zinazoelezwa ndani ya Yanga baada ya Kocha George Lwandamina kuondoka klabuni hapo na kurejea Zesco United, ni kutokuwa na mahusiano mazuri baina yake na Katibu Mkuu wa timu, Charles Boniface Mkwasa.
Inasemekana kuwa Lwandamina hakuwa ana maelewano mazuri na Mkwasa haswa katika masuala ya utendaji wa klabu hivyo inatajwa ikawa sababu ya yeye kuondoka na kutimkia kwa Zambia.
Zipo taarifa za chini ya kapeti zinazosema Mkwasa alikuwa akihitaji kuchukua nafasi yake ya ukocha na aachane na wadhifa wa Ukatibu Mkuu alionao kwa sasa.
Kuafuatia hayo yote kutokea, Katibu Mkuu wa Mashindano ya Yanga, Samuel Lukumay, amesema Kamati ya Utendaji itakaa baada ya mchezo wa leo dhidi ya Singida kutoa tamko rasmi kama klabu kuhusiana na kuondoka kwa Lwandamina.
Lwandamina ameondoka Yanga ikiwa inajiandaa na mchezo wa ligi pamoja na mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Wolaitta Dicha FC.
Tuseme ukweli kuwa Mkataba na Lwandamina umekwisha ndio maana hata yeye mwenyewe alikuwa tayari kuondoka Yanga na si vinginevyo. Suala la Mkwasa kuchukua nafasi ya kuifundisha Yanga angeweza hata kabla ya Lwandamina kuja Yanga. Mbona aliondoka Babu???
ReplyDeleteTuseme ukweli kuwa Mkataba na Lwandamina umekwisha ndio maana hata yeye mwenyewe alikuwa tayari kuondoka Yanga na si vinginevyo. Suala la Mkwasa kuchukua nafasi ya kuifundisha Yanga angeweza hata kabla ya Lwandamina kuja Yanga. Mbona aliondoka Babu???
ReplyDeleteZipo habari nyeniine zataja mojawapo ya sababu ya kuingia mitini ni kutolipwa mshahara kwa muda wa miezi mitatu
ReplyDeleteNasikia Chirwa pia yupo njiani kuelekea Simba
ReplyDeleteKila la kheri kwa wanaondoka na wanaokuja kurithi mikoba kwani yote ni maisha.
ReplyDeleteAcha Uwongo Sababu Ni Hizi
ReplyDeletea)MSHAHARA
b)EMMANUEL OKWI
c)NJAA
d)KARIAKOO DABI