April 19, 2018




Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amesema wao hawana hofu hata kidogo na mechi dhidi ya watani wao Simba.

Simba itakutana na Yanga katika mechi ya Ligi Kuu Bara itakayopigwa Aprili 29 jijini Dar es Salaam.

Mkwasa amesema anaamini kama ni maneno, basi watani wao Simba wangekuwa na nafasi ya kuwa mabingwa kwa kuwa “wanachonga” sana.

“Suala la kutishia kutufunga ni hadithi tu, mpira hauko hivyo. Unajua wenzetu wanaongea sana, maana kama ingekuwa kuna kombe la kuzungumza, basi wao wangekuwa mabingwa.

“Tuna timu nzuri na tunaweza kupambana na kufanya vizuri, hakuna masuala ya kusema utafungwa na mwingine kujiamini kwa asilimia mia atashinda,” alisema.

Mashabiki wa Simba ndiyo walikuwa wanatamba kwa muda mrefu kutokana na kasi ya kikosi chao katika Ligi Kuu Bara, lakini Yanga wamepata morali baada ya kikosi chao kuingia katika hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa kuing’oa Wolayta Dicha ya Ethiopia.

10 COMMENTS:

  1. Ningeliwasifu kama mngepata ushindi Ethiopia, lakini mmefungwa sikusifuni na huo ushindi wa bahatinasibu na si wa uwanjani ni ushindi usiokuwa na utamu hata kidogo na mmepata pesa bila ya jasho la ushindani na nyumbani ndio mnangojewa kuonesha kama kweli ulikuwa mmepta ushindi wa heshima

    ReplyDelete
    Replies
    1. Unachanganya mambo, mbona na nyie hamkupata huo ushindi wa kubahatisha ilu msonge mbele!? Huo ni wivu wa kizamani na ulimbukeni!!

      Delete
    2. Huu unaitwa wivu wa mke mwenza......! Kwani AS Roma kafikaje Nusu Fainali ya UEFA? Kama hujui mtindo wa mechi za nyumbani na ugenini kaaa kimya

      Delete
  2. Mkwasa yupo sahihi kabisa yanga wana Timu nzuri tena sana tu lakini watafungwa na Simba. Kama mechi hiyo ingekuwa inachezwa mikoani Yanga angekuwa na nafasi ya kushinda lakini bahati mbaya kwao yanga mwchi hiyo itachezwa Daresalam Simba inakuwa ni timu yenye moral wa kujiamini zaidi inapocheza Daresalam Kuna wakati fulani kocha Mholanzi Puijm aliwahi kusema Simba huwafungi Daresalam. Hakuwa anasema hivi hivi tu bali kuna sababu za kiufundi zilimpelekea kutoa kauli ile.

    ReplyDelete
  3. Wameishinda timu iliyo nafasi ya tisa katika premium league Ethiopia

    ReplyDelete
  4. Wameishinda timu iliyo nafasi ya tisa katika premium league Ethiopia

    ReplyDelete
  5. Mashindano ya Kimataifa yana mbinu na mfumo wake si kama ligi ilivyo. Ligi unaamini ukipoteza hapa utapata pale. Mashindano haya ya mtoano hayana mantiki endapo utashinda alafu utolewe. Kwahyo tunachokiangalia si kufunga ila ni kufuzu kwenda kwenye hatua nyingine. Kulinda ushindi inahitajika akili ya ziada kweli kweli na si kukurupuka kwenda kufanya kitu mnachofikilia. Wakati wa mtoano hauhitaji mpira mzuri ila mnahitaji mbinu ya kuwatoa timu pinzani. Walicheza mpira mzuri Barcelona lakini unaweza wauliza sasa wapo wapi. Kikubwa si kuwafunga...ila ni kufuzu

    ReplyDelete
  6. Tabga imenishinda timu inayotoka ya 9 katika moja ya ligi dhaifu zaidi ktk ligi za Africa ndio maana timu zote za ethiopia zimetolewa sababu ligi hai ni dhaifu zaidi Africa

    ReplyDelete
  7. Ligi ya Ethiopia ni moja ya ligi dhaifu zaidi ktk Africa. Haina tofauti na ligi ya Botswana. yanga zimecheza na timu ya 9 katika ligi hiyo. Tena timu ambayo haijawai chukua ubingwa kwenye ligi hiyo dhaifu. ubora halisi wa yanga utaonekana tarehe 29 kama kweli ni bora

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic