April 19, 2018



Na George Mganga

Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Naseeb Abdul, 'Diamond Platnumz, amemtumia salaam mwanamziki mwenzake, Ali Kiba ambaye amefunga ndoa na mchumba wake Amina Khaleef, mjini Mombasa Kenya.

Alikiba amefunga ndoa na Bi Amina mapema leo asubuhi katika msikiti wa Ummul Kulthum huku ikishuhudiwa na baadhi ya viongozi ikiwemo Gavana wa Mobasa, Hassan Joho.

Katika salaam hizo ambazo amemtumia Kiba, Ptanumz amemuita Diamond kuwa ni Mfalme kama ambavyo amekuwa akijiita tangu arejee tena kwenye soko la muziki baada ya likizo yake ya miaka mitatu.

Mbali na kumita Mfalme 'King Kiba', Diamond amemtakia kila la kheri katika maisha mapya ya ndoa yaliyo na furaha pamoja na amani.



2 COMMENTS:

  1. Saleh Mwambie Huyo George sio Ukumbi wa Ummul Kulthum ni Msikiti wa Ummul Kulthum...asipotoshe watu...

    ReplyDelete
  2. Asa kwani George kakosea wapi?au ndio nyie timu wehu??

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic